Jana 11 Mei 2021 Jumanne waislam duniani wengine walikuwa siku ya 29 wengine 28 kwa hivyo wale wanaofuata mwezi wa kimataifa walikuwa wanaangalia muandamo wa mwezi.
Kwa upande wa Saudia haijatoka taarifa yoyote ya kuonekana kwa mwezi kwa hivyo Serikali yao imetangaza kuwa eid itakuwa Siku ya Alhamisi 13 Mei 2021.
Waislam huanzaga kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan kutokana na kuonekana kwa mwezi katika maeneo yao au popote duniani kulingana na misimamo ya maulamaa tofauti .
Ramadhan ya mwaka huu ilikuwa na changamoto mbalimbali kutokana na hali ya uchumi kuyumba duniani na mzunguko wa pesa kuwa bado uko chini.
Tunawatakia waislam wote maandalizi mema ya sikukuu ya #eidelfitr .
Muda huu waislam wanachakarika kula kona ya dunia kuandaa zakka na kisha baada ya Ramadhan huwaga wana siku sita za Shawwal (month) ambazo kuzifunga kunafanya sawa na kufunga siku 60 ambapo ukijumuisha na funga ya Ramadhan wanaandikiwa sawa na kufunga mwaka mzima.
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email
No Comments