Saturday, May 15, 2021

thumbnail

MAKAMPUNI MAKUBWA KUMI YANAYOTOA MITAJI KWA VIJANA NA WAJASIRIAMALI AFRICA.-KINDAMBA MULTIPURPOSE

Unatafuta mtaji 2021/2022 kwa biashara yako Africa?

                                      

https://www.thesmallbusinesssite.co.za/wp-content/uploads/2019/03/funding.jpg

Umejaribu njia mbalimbali kupata mtaji lakini haujafanikiwa? 

Je mtaji ndo kitu kikubwa kinachopasua kichwa chako hivi sasa?

Hizi hapa taasisi kumi zinakutoa katika shida yako :

1) Seedstars Africa

Seedstars wamewekeza katika nchi si chini ya 65 duniani. Seedstars wanaandaaga mashindano ambapo wajasiriamali hujitokeza na kwenda kushindana kuwakilisha idea zao.

Seedstars huwaga wanaendesha mashindano kama 65. Mashindano hayo huangalia nani anakuja na wazo bora sokoni. Washindani hufundishwa jinsi ya kujielezea na washindi hupewa zawadi.

Mwaka 2019, Argentinian edtech walitangazwa washindi wao wa dunia nzima na wakapewa dollar $500,000 za kimarekani.

2) Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Program

Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme (TEEP) hii ni program ya kila mwaka yenye makusudio ya kutoa mafunzo, kuwezesha(fund), na kutoa motisha kwa wajasiriamali wa AFRICA.

Imegunduliwa na  Mr. Tony Elumelu, mnaijeria huyu mwenye mafanikio katika ujasiriamali na kutoa misaada, nia yake ni kuwasaidia wajasiriamalia 1000 kila mwaka katika miaka kumihii tunayokwenda nayo.

kila aliyefanikiwa kushiriki anapata $5000 za kimarekani kama uwekezaji wake baada ya semina ya wiki 12 dola nyingine $5000 hupewa kama mkopo kwa wale wanaokidhi vigezo.

katika miaka kumi taasisi hii inakusudia kutoa mitaji kwa wajasiriamali 10,000 ambayo itazalisha ajira mpaka milioni moja kutokana na wao na mapato ya $10 bilion dollar kuingizwa katika Africa kupitia fursa hizo.

TEEP inawakusudia hasa wakazi wa Africa katika nchi zote 54.

TAASISI NYINGINE NI 

3) African Women’s Development Fund (AWDF)

AWDF Tangu kuanza kwa shughuli zake mnamo 2001, AWDF imetoa msaada wa dola milioni17 kwa mashirika 800 ya wanawake katika nchi 42 za Afrika.

AWDF inatoa ruzuku kwa makampuni tu wala sio watu binafsi, na hutoa pesa  $8,000 mpaka $50,000.

4) Acumen Fund

Acumen ni taasisi ya misaada inayofadhiliwa na  Rockefeller Foundation, Cisco Systems Foundation na watu watatu wengine binafsi (philanthropists).

wamekwisha wekeza $115 million katika makampuni 113 na huwa wanawekeza katika sekta tofauti tofauti.

5) CDC

CDC is the UK’s Development Finance Institution (DFI) inayomilikiwa kabisa na Idara ya Serikali ya Uingereza ya Maendeleo ya Kimataifa(DFID).Ni DFI kongwe zaidi ulimwenguni na historia ya kufanya uwekezaji wenye mafanikio katika biashara ambazo zimekuwa viongozi wa tasnia.

6) Bill and Melinda Gates Foundation

The Bill & Melinda Gates Foundation ni taasisi binafsi ya misaada iliyogunduliwa na bill Gates pamoja na aliyekuwa mkewe, Melinda Gates.

ilianzishwa mwaka 2000 na ndiyo taasisi binafsi yenye mafanikio makubwa zaidi kulikoo zote duniani , mpaka kufikia december 2014 ilikuwa imezalisjha $44.9 za kimarekani.

Taasisi hii ina ofisi tatu Africa zilizopo  Ethiopia, Nigeria, na  South Africa, nchi ambazo shea zake na uwekezaji wake mkubwa umefanyika humo. hata hivyo kama ulikuwa hujui, basi taasisi hii imefika pia  Kenya, Tanzania, Ghana, Senegal, Zambia, na Burkina Faso.

2016, taasisi hii ilitoa ruzuju $4.48 million dollar kwa  Sidai Africa, kampuni ya kijamii inayofanya kazi katika sekta ya ufugaji KENYA.

June 2017, TAASISI HII ILITOA  $2.4 million Kama ruzuku kwa  Sanergy, taasisi inayotoa misaada na fursa kwa watu wa vijijini.

taasisi nyinginezo ni

7) IFC

 International Finance Corporation,

8) Helios Investment Partners

 Helios Investment Partners

9) Norfund

Norfund

10) TL COM Capital

 TLcom Capital LLP .

ZINGATIO:

Kupata fursa ya uwekezaji au pesa kutoka kwenye makampuni haya si kazi rahisi.  ingawa kama unafa mifumo mizuri na unajua kipi unatakiwa kufanya inakuwa kuna wepesi kidogo.kwahiyo cha msingi pitia nini kinachotakiwa kufanywa na jiandae ili unapokutana na fursa kama hizi zisikupite. endelea kuwa karibu nami upate maarifa mengi zaidi.


Related Posts :

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

Copyright © 2021, Haki Zote Zimehifadhiwa. | Content by hafidh kindamba. Powered by Blogger.