
Kwa mara nyingine tena , karibuni sana tuendelee kupata masomo mbalimbali kuhusu ujasiriamali. Mara zote mimi nikitoa masomo ya ujasiriamali huwa si tu ninatoa maelezo bali utafiti wangu unaingia kwa kina sana kiasi kwamba mimi mwenyewe huwa ninaingia katika uwanja wa kufanya kivitendo ili nione matunda na hasara ya kitu ambacho nikija kukuelezea wewe ndugu yangu upate faida kamili.
Ujasiriamali katika biashara ya kuuza kripsi hauhitaji mambo mengi zaidi ya akili yako, afya yako na mtaji kidogo tu na kujifunza zaidi kutoka kwa wengine kuwa wanafanya vipi aidha kwa kuuliza au kufatilia vitendo vyao.
Kwa hiyo tafuta mtaji wako hata shilingi alfu ishirini inakutosha kuanza ujasiriamali huu kwa siku ya kwanza. Utanunua mihogo ya alfu tano, jitahidi ujue sehemu za sokoni vizuri. kisha utanunua mafuta hata ya lita moja , kwa sasa lita moja ni 3,000-5,000 utanunua na viazi, pia utanunua mashine ya kukatia krips ambazo zinapatikana mjini ila kuwa makini mana nyingine hazidumu muda mrefu na ukikurupuka unaweza kutajiwa bei kuwa mana wafanyabiashara tofauti tofauti.
Mimi nilipita maduka mengi sana kabla ya kujiridhisha bei yake na nilipata kwa shilingi 12,000 original mwingine hikohiko nikakuta anauza 25,000 na yuko serious hapunguzi bei.
Kisha utanunua vifuko vya kufungia crips size 5x10 vinakaa 50 au mia bei yake 1800, utanunua vibeseni utakavyovitumia kukaangia na kwenda kuuza kama barabarani. chujio utachagua kama ni la alfu kumi au dogo lake. utanunua mkaa , na karai unaweza kuanza kutumia hata la nyumbani . hapa nimekupa elimu kwa ufupi. lakini kama unataka kuifanya biashara hii kama ni mradi mkubwa, unaweza kutafuta vijana na kuongea nao ukawalipa commission kwa kila crisps watakayouza.
kwa maelekezo zaidi mpaka kufanikisha mradi wako wa biashara hii, mimi mwenyewe ninaweza kukupa mafunzo kivitendo mpaka biashara inasimama vizuri.
Unaweza ukawa wewe hauendi kuuza lakini ukawa unasimamia biashara tu, mimi siogopagi kuthubutu kwa hiyo hata hapa ninatoa ushuhuda kuwa niliifanya hii kivitendo na ni mbinu ndogo ndogo tu zlizonifanya niwe wa kipekee.
Ikiwa unataka kuonana nasi tukupe somo hili kwa ukamilifu unaweza tupigia kwa nambari 0685303727 au 0713225702
usisahau kufollow page hii, na instagram ni @KINDAMBA_MULTIPURPOSE
6:59 AM
Tags :
EDUCATION
,
ENTREPRENEURSHIP
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email
No Comments